Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi leo katika kikao cha kawida cha baraza wamepitisha kwa kauli moja azimio kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia Halmashauri hiyo kupewa zaidi ya shilingi Bilioni tatu ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotolewa katika kupambana na Changamoto za UVIKO 19
Mwenyekiti wa baraza la madiwani Mhe Aliy Juma Mwanga akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza amesema Halmashauri imepokea ya shilingi bilioni 2.6 fedha za ujenzi wa madarasa 67 mapya ya shule za secondary na madarasa 65 mapya ya shule shikizi za msingi na zaidi ya milioni 860 kwenye miradi ya maji
Mhe Mwanga amesema fedha hizo ni nyingi ambazo zilikuwa nje ya bajeti ya Halmashauri na kwa pamoja wamemuomba Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry Muro ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao cha baraza kufikisha salamu na azimio la pongezi la madiwani kwa Mhe Rais, Samia Suluhu Hassan
Akizungumza wakati wa kupokea azimio hilo, mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry Muro amesema Serikali ya awamu ta sita itaendelea kupeleka fedha za miradi ya Maendeleo kama ambavyo imelekezwa katika ilani ya chama cha mapinduzi na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kutafuta vyanzo vipya vya fedha kwa ajili ya kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za kijamii
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa