Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego aipongeza Wilaya ya Ikungi kwa kuandaa bonanza la michezo lenye adhma ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao Novemba 27, 2024 nchini kote.Mkuu wa mkoa amezungumza hayo hii leo tarehe 05 Octoba, 2024 katika Bonaza lililofanyika kijiji cha Makiungu kata ya Mungaa katika viwanja Mungaa sekondari.Mhe. Dendego ameongeza na kusema kuwa vijana washiriki katika michezo mbalimbali kwani ni chanzo cha ajira na ni afya pia."Nitatoa zawadi ya shilingi elfu 20 kwa kila goli litakalofungwa lengo ni kuhamasisha michezo katika mkoa wetu" Amezungumza DendegoKwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson amesema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu kwani ndiki tunakokwenda kupata viongozi tunaoishi nao katika vijiji vyetu na mitaa yetu hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili kuchochea maendeleo yetu kwa kuwachagua viongozi sahihi.kwa upande wao wachezaji pamoja na baadhi ya wananchi mara baada ya mchezo huo wamezungumza na kusema kuwa wanapongeza viongozi kwa kuandaa michezo hiyo na wanaomba iwepo mara kwa mara kuimarisha afya zao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa