Katibu tawala wa wilaya na mwenyekiti kamati tendaji ya maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru yanayotarajiwa kufannyika tarehe 9 mwezi huu Bi Winfrida Funto amewaongoza watumishi wa wilaya ya Ikungi kupanda miti katika mazingira ya Nyumba za watumishi na maeneo katika mbalimbali wilayani hapa.
Akizungumza na watumishi kabla na baada ya kupanda miti hiyo leo tarehe 06 Desemba, 2022 Bi Winfrida amesema kuwa ni wajibu wao kutunza mazingira na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha miti inapandwa katika kata zote wilaya ya Ikungi.
Aidha Winfrida ameongeza na kutoa maagizo kuwa siku ya kesho tarehe 07 Desemba,2022 saa 07:30 kila mtumishi afike shule ya msingi Ikungi kwa ajili ya kufanya usafi na kupanda miti kwa ajili ya kuweka mazingira safi.
Pia katika kilele cha maadhimisho hayo katibu tawala wa wilaya amesema ki wilaya yatafanyika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi na kila mmoja anakaribishwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa