Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Leo Tarehe 24 Octoba 2023 imezindua rasmi Msimu wa Kilimo 2023/2024Katika uzinduzi huo mgeni rasmi Diwani wa kata ya Issuna Mhe Stephano Misahi ambaye amemwakilisha Mhe Mkuu wa wilaya ya Ikungi, amewahamasisha washiriki kuendelea kutenga maeneo makubwa zaidi kwa ajili ya kilimo cha Pamba kwani kina tija na kinakubalika katika mazingira yetu.Pia Mhe mgeni rasmi ameongeza kwa kusema mazao ya kimkakati katika wilaya yetu ya Ikungi imeyataja kati ya matano ni alizeti,korosho na Pamba kwani kupitia hayo yatamkomboa mkulima wa Hali ya chini.Pia katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi amesema kuwa malengo ya Halmashauri ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara sambamba na mazao ya mbogamboga na matunda.Ameongeza kwa kusema kuwa tumekusudia kulima hekta 161,234.15 za chakula na mavuno yawe Tani 338,96na mazao ya biashara hekta 86,171 na mavuno Tani 124157.1 pamoja na mbogamboga hekta 350 na mavuno yawe Tani 548.Aidha serikali inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan inalenga kumkomboa mkulima kwa kusisitiza kutumia mfumo wa stakabadhi mazao Ghalani ili mkulima kupata ushindani wa bei na kuuza mazao yake kwa tija.Mwisho washiriki wa hafla hiyo wamesisitizwa na wadau tofautitofauti kutumia mbegu kutokana na mazingira na hali ya hewa kwa kipindi husika cha msimu,kukopa kwaajili ya mashamba kupitia banki,kujisajili kwenye daftari za ruzuku ya mbolea lengo mbolea ifike kwa wakati.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa