Wabunge wa Majimbo ya Singida Mashariki na Magharibi Mhe Jumanne Miraji Mtaturu na Elibariki Kingu wamekabidhi magari mawili aina ya landcruser kwaajili ya huduma za haraka (Ambulance) katika hospitali ya Wilaya ya Ikungi na kituo cha afya Sepuka ili kurahisisha huduma za afya kwa wagonjwa walio zidiwa .Wakizungumza katika makabidhiano hayo leo Tarehe 04 februari,2024 Mhe Mtaturu amesema kuwa serikali imetoa magari hayo katika wilaya ya Ikungi kwa madhumuni ya kuepusha vifo vitokanavyo na kucheleweshwa kwa wagonjwa pale wanapozidiwa ."Zaidi ya milioni 140 zimetumika kununua gari mmoja hivyo serikali imeipa kipaumbele sekta ya afya kwa madhumuni pia ya kuepusha vifo vya mama na mtoto"Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe amesema kuwa wapo tayari kushirikiana na mganga mkuu na mganga mfawidhi kuhakikisha magari yanatunzwa na kutumiwa kwa malengo mahususi ya kubeba wagonjwa.Baadhi ya wananchi walio hudhuria katika makabidhiano hayo wamesema kuwa wanamshukuru Raisi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali wananchi wa Ikungi kwa kuletwa kwa huduma hii ya Ambulance katika hospitali ya Wilaya. Mwisho Mhe Mtaturu ameomba gari lililokuwa likitumiwa mwanzo litumike katika kituo cha Afya cha Ntuntu kutokana na umbali wa kituo hicho kilipo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa