Mradi wa Kuboresha miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira SWASH wapokea milioni 61.8 inayoelekezwa kuboresha miradi ya maji,Vyoo vya Shule za Msingi na kuboresha zahanati hasa upande wa vyoo na Vichomea taka katika Wilaya ya Ikungi.Hayo yamesemwa leo Tarehe 11 Januari 2024 katika kikao cha uhabarisho Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Afisa Afya Halmashauri wa Wilaya ya Ikungi Ndg Abiudi Abiudi amesema kuwa kipaumbele cha fedha hizo zitapelekwa katika ujenzi wa Vichomea taka Zahanati ya Mgungira na Ng'ongosoro na kufanya ukarabati wa zahanati hizo Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amesema amefurahishwa na Idara ya Afya katika ushirikishwaji wa fedha za miradi zinazoelekezwa katika Wilaya ya Ikungi kwani inarahisisha usimamizi wa Miradi hiyo kulingana na thamani yake."Kipaumbele chetu kama Wilaya tulenge kwenye umaliziaji wa viporo vya miradi iliyosalia ili tukianza miradi mpya tusiwe na viporo."Amesema Mkuu wa Wilaya.Aidha mradi unalenga pia kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya mlipuko kama vile Kipindupindu,Korona na magonjwa yote ya Mlipuko kuepusha vifo vinavyoweza kutokea.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa