Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imepokea jumla ya vishikwambi 1,496 kwa ajili ya kuwapatia walimu pamoja na Maafisa elimu Msingi na Sekondari kwa awamu mbili...
Akizungumza katika zoezi hilo la kugawa vishikwambi kwa walimu wa sekondari na shule ya msingi tarehe 23 Januari Katibu tawala wa Wilaya Ikungi Mhe Winfrida Funto amesema kuwa vishikwambi vitumike vizuri kukuza taaluma katika wilaya hii...
Aidha tarehe 08/12/2022 Idara ya Elimu msingi ilipokea jumla ya vishikwambi 653 na Idara ya Elimu sekondari imepokea 306 kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili tarehe 22/01/2023 idara ya elimu sekondari imepokea jumla ya vishikwambi 208 na idara ya elimu msingi vishikwambi 329...
Ambapo jumla ya vishikwambi vilivyopokelewa kwa idara ya elimu msingi na Sekondari kwa awamu zote mbili ni jumla ya vishikwambi 1,496.
Mwisho
Afisa Habari
Halmashauri (W) Ikungi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa