Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg.Justice L.Kijazi afungua mafunzo yakuboresha utendaji kazi kwa madiwani na wakuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mafunzo hayo yameanza hii leo tarehe 16 Disemba, 2024 mpaka 20 Disemba, 2024 ambapo Halmashauri imeandaa mafunzo ya ujazaji tamko la maadili kwa viongozi kufuatia matakwa mapya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ya ujazaji wa tamko la rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma kwa njia ya mfumo kwa mujibu wa sheria.
"Tumealika viongozi kutoka taasisi mbalimbali ili kutoa mada kuhusu uboreshaji utendaji kazi wetu hivyo tutakuwa na mada kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU na tamko la rasilimali na madeni na masuala ya serikali za mitaa" amezungumza Kijazi
Mkurugenzi Mtendaji ameongeza na kusema kuwa mwisho wa kujaza Tamko la maadili ni tarehe 31 Disemba, 2024.
Aidha Halmashauri imeandaa bajeti kwa mafunzo hayo ya siku 5 ili kuwawezesha viongozi hao kujifunza maswala ya utawala bora kwa maslahi mapana ya wananchi wa wilaya ya Ikungi na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe katika mafunzo hayo wameishukuru Halmashauri kwa kutenga bajeti kwa ajili ya mafunzo hayo kwani yanaenda kuwa chachu katika utendaji kazi katika maeneo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa