Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Ndg Jerry Muro akiongozana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Richard Rwehumbiza pamoja na Afisa Elimu awali na msingi Wilaya ya Ikungi Bi Margaret K.Kapolesya amefanya uzinduzi wa vitabu vya mpango endelevu wa mafunzo ya walimu kazini (MEWAKA)…
Uzinduzi huo umefanyika hii leo tarehe 29 Septemba 2022, shule ya msingi Ikungi alipokua akizungumza na Maafisa Taaluma, Wathibiti ubora wa shule, Walimu wakuu ,Walimu wa taaluma na Walimu mahiri shule za msingi zilizopo Wilaya ya Ikungi wanaoendelea kupata mafunzo ya walimu kazini (MEWAKA) chini ya wataalamu kutoka wizara ya elimu (WEST) na Wakufuzi wa vyuo vya ualimu CAMBRIDGE Mradi wa shule bora na kusema kuwa andiko hilo limeandikwa kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu nchini na kuwataka wazingatie wanachofundishwa .”Nawapongeza kwa kujitoa na kuwa na utayari wa kujifunza” alisema Muro…
Aidha Muro mewaomba walimu kuyafanyia kazi na kutekeleza yale wanayofundishwa kupitia wakufunzi pamoja na nakala za vitabu vilivyozinduliwa kwa ajili ya mafunzo hayo,”Mkisoma na kuvielewa mnaweza kuboresha zaidi katika kufundisha na ujifunzaji wa wanafunzi Mkuu wa Wilaya hiyo alisema…
Aliongeza na kusema kuwa vitabu hivyo vinabainisha hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kuboresha elimu nchini ili kuondoa changamoto zinazokwamisha ujifunzaji shuleni...
Mafunzo ya mpango edelevu ya walimu kazini MEWAKA yatafanyika takribani siku tano katika shule ya msingi Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa