Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amepongeza kazi nzuri ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Mhe.Jafo alitoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Wilayani humo ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ambapo akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na usimamizi, ubora na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ihanje.
Aliongeza kuwa Kituo cha Ihanje ni miongoni mwa Zaidi ya Vituo 200 vitakavyopekea/vilivyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya ambayo ilikosekana hapo awali na kukifanya kituo hiki kutotoa huduma ipasavyo na agizo langu la awali ilikua kumaliza kazi ya ujenzi mnamo Dec 30,2017 lakini kwa Ikungi walichelewa kuanza utekelezaji kutokana na kupokea maelekezo mengine baadae ila wamefanya kazi nzuri hivyo wao watakamilisha Jengo hili mnamo January 2018.
Nimekagua majengo yote sita yanayojengwa kupitia uboreshaji huu hakika yanavutia na kupendeza, kuanzia Maabara, Wodi ya Kinamama, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia Maiti pamoja na kichomea Taka na ukizingatia ujenzi huu umewahusisha mafundi kutoka kwenye Vijiji na Kata zetu ambapo kwa kuwatumia wao gharama za ujenzi hupungua ukilinganisha na wakandarasi; Hii inanipa faraja kubwa kuona kazi zinaenda vizuri kutoka kwa watalaam walioko kwenye jamii yetu, Alisema Mhe.Jafo.
Awali akitoa taarifa hiyo Mhandishi wa Ujenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Sembua Mrisho amesema Fedha zilizopokelewa ni Tsh. Mil 720 kati ya hizo Mil 220 zimepelekwa bohari ya dawa kwa ajili ya vifaa Tiba na Dawa mara majengo hayo yatakapokamilika na Tsh Mil 500 ndizo zinazotumika katika Ujenzi wa miundombinu yote sita na hali ya ujenzi mpaka sasa inaonyesha Fedha hizo zitakamilisha kabisa mradi huo kwa ubora unaotakiwa.
“Mara baada ya kupokea Fedha hizo na kupata Muongozo toka OR-TAMISEMI, Fedha zile zililetwa kwenye Kata na zikaundwa kamati Tatu ya Mapokezi, Manunuzi na Ujenzi na kazi yote hii imefanyika kwa kutumia “Local fund” na inasimamia na Wakandarasi wa Halmashauri kwa kushirikiana na kamati za Ujenzi zilizopo” alisema Mrisho.
Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mbunge wa Ikungi Mhe.Elibariki Kingu amesema Ihanje ni Kata pia ni Makao Makuu ya Tarafa ya Ihanje na mradi huu umejibu shida za wananchi wa Ihanje na Ikungi kwa Ujumla kwa sababu Kituo hicho kinatoa huduma kwa wakinamama wengi wa Kata zaidi ya Tano zinazonguka eneo hili.
Aliongeza kuwa Kituo cha Afya kilichkuwepo awali kilikuwa hakikidhi mahitaji kutokana na kutokua na maeneo muhimu kama wodi nzuri na kubwa ya kina mama, maabara, sehemu ya kuhifadhia maiti nk lakini kwa sasa sisi wananchi wa Ikungi tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kututatulia hangamoto hii.
Akizungumza kwa furaha Angelina Naaman(Mama Yasinta) amesema “Wakinana mama sasa tutaona raha Zaidi ya kujifungua kwa sababu tumepata mpaka chumba cha Upasuaji wakati awali ilikua ukishindwa kujifungua kawaida inakua mtihani sana kwako na kwa wauguzi wenyewe hivyo sasa zoezi la kujifungua kwetu litakua salama Zaidi kwa masiah yetu nay a mtoto.
Ukarabati sambamba na uboreshaji wa vituo vya Afya vinavyoendelea Nchini Kote utafanyika katika awamu na awamu ya kwanza ilianza Mwezi Sept 2017 na utakamilika January, 2018 na umehusisha vituo 44 wakati awamu ya Pili itaanza mwenzi January 2017 utahusisha Vituo vya Afya 161
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa