Jeshi la polisi Mkoa wa Singida Wilaya ya Ikungi wafanya usafi na kubeba mchanga kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo yatakayotumiwa na wanafunzi wenye uhitaji maalumu shule ya Msingi Ikungi.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi Bi-Susana Kidiku leo tarehe 14 January 2023 amesema kuwa wamejitoa kuwasaidia mafundi ili mabwalo yakamilike kwa wakati kusudi watoto wasome na kupumzika katika hali ya utulivu."tumefanya hivi kwa dhumuni la kumhakikishia mazingira bora mtoto mwenye uhitaji maalumu na kusaidia kuongeza kiwango cha ufaulu,na zoezi hili ni endelevu kadri tutakapopata nafasi ya kusaidia shughuli mbali mbali za kijamii tutafanya hivyo"Alisema mkuu wa polisi.
Kwa upande wao watoto wenye uhitaji maalumu wameishukuru serikali hasa viongozi wa wilaya kwa kufikiri ni vyema kuwaletea majengo hayo na kuwafanya wasome kwa bidii."naomba serikali ituongeze vifaa pia vya kujifunzia pamona na walimu"Alizungumza mmoja wa wanafunzi.
Mkuu wa polisi alitoa wito kwa wananchi na kuwahimiza kujitokeza kusaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kukuza Maendeleo kwa kazi katika wilaya ya Ikungi.
Tazama Picha za Matukio
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa