Kamati ya Bunge Tawala za Mikoa na serikali za mitaa yaridhishwa na utendaji kazi wa viongozi wa wilaya ya Ikungi na kuwapongeza kwa kuisadia serikali kukamilisha baadhi ya miundombinu iliyopelea baada ya fedha zilizobaki kurudishwa hazina ili hospitali iendelee kutumika...
Hayo yamesemwa leo Tarehe 19 Machi 2023 na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge Mhe Denis Londobaada ya kamati hiyo kutembelea majengo mbalimbali ya hospitali hiyo na kuridhishwa na ujenzi huo "kwa niaba ya kamati niwapongeze viongozi wa Ikungi na haya ndiyo maamuzi ya kiuongozi,fedha kweli zilikuja na maelekezo ila nyie mkajiongeza kwa kukamilisha majengo muhimu ili huduma zianze kutolewa nawapongeza sana" Alisema Mwenyekiti wa kamati ya Bunge
Aidha kamati ya Bunge imeagiza fedha zilizorudishwa Hazina ziletwe ili kukamilisha ujenzi unaoendelea katika hospitali hii."sisi kama kamati tunaongezea uzito wa maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majali pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Mhe Daniel Chongolo walipotembelea hospitali hii hivi karibuni,Fedha zilizorudishwa Hazina ziletwe haraka kukamilisha Hospitali hii.Amezungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba ameiambia kamati ya Bunge kuwa Wilaya ya Ikungi ni miongoni mwa wilaya 6 Katika mkoa huu na ndiyo inayoongoza katika ukamilishaji wa miradi mapema kama Serikali inavyoagiza."sina mashaka na utendaji kazi wa Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa wilaya fedha zikiletwa Majengo yote yatakamilika kwa wakati.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa