Kamati ya Fedha halmashauri ya Wilaya ya Ikungi yatembelea miradi ya SWASH katika zahanati tatu 3 zilizopo Kijiji cha Nkuhi,Dungunyi pamoja na Matyuku na kubaini miradi hiyo kwa asilimia kubwa imekamilika.
Akizungumza katika ukaguzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Aliy J.Mwanga amesema kuwa ujenzi umekalika Nkuhi kwa asilimia 96 Dungunyi asilimia 100 na Matyuku ni asilimia 100 ila mfumo wa maji unahitaji marekebisho madogo na kutoa maagizo kuwa vyoo vilivyokamilika vianze kutumika mara moja ili kuepukana na adha wanazopata wagonjwa kipindi wapo katika kupata matibabu kwenye zahanati hizo...
Mhe Mwanga ameongeza na kusema kuwa miundo mbinu ambayo inatolewa ni muhimu itunzwe na kuthaminiwa ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu...
Aidha repoti ya mradi huo wa SWASH unaonyesha Zaidi ya 23,90,000/= zimetumika Zahanati ya Nkui kujenga vyoo,Dungunyi 20,000,000/=
na Matyuku ni Shilingi 25,000,000/= ambapo imesaidia kukamiliza matundu ya vyoo na mfumo wake wa maji.
MWISHO
________________________________
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
24/01/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa