Kamati ya fedha mipango na uratibu yatembelea hospitali ya wilaya ya ikungi Leo 26 Octoba 2023.Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati ya fedha mipango na uratibu Mhe Mtyana Petro ameridhishwa na majengo hayo mapya ambayo ni jengo la mama na mtoto ,wodi ya wanaume ,wodi ya wanawake pamoja na mochwari na kusema kuwa Sasa wahudumu wa afya waongezwe ili wagonjwa waanze kupata huduma ya malazi.Pia mwakilishi wa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Ikungi amesema kuwa huduma zote za hospitali kwa Sasa zipo na waameanza kuhudumia wagonjwa kwa masaa 24 ,kilichobaki ni hizo wodi kutokutoa huduma kwa sababu ya upungufu wa wahudumu hapo hospitalini.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa