Kamati ya fedha, Uongozi na mipango ya Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi yatembelea mradi wa ujenzi wa maduka katika stendi ya Ikungi na kumuagiza mkandarasi ujenzi huo kukamilika kwa wakati ili stendi hiyo ianze kutumika rasmi.
Akisoma taarifa ya mradi huo mhandisi wa Wilaya ya Ikungi amesema kuwa mradi huo wa maduka 20 ni mradi wa fedha za uajibikaji kwa jamii CSR kutoka kampuni ya uchimbaji madini SHANTA GOLD MINING wenye thanani ya dola za kimarekani 69,000sawa na shilingi za kitanzania milioni 175
Hata hivyo alisema mradi huo unatekelezwa kwa kutumia mkandarasi na muda wake wa utekelezaji ulikua ni jumla ya miezi mitatu kuanzia tarehe 05 Octoba, 2024 mpaka 05 Januari 2025 kwa sasa ujenzi upo hatua ya lenta.
Kamati hiyo imejadiki kutokuridhishwa kwa kasi ya ujenzi huo na kuwataka waliochukua tenda hiyo kujibu sababu zinazochelewesha ujenzi huo ambao mpaka sasa ulipaswa uwe kamili Kwa upande wake mkandarasi wa ujenzi huo amesema kuwa changamoto kubwa imekuwa ni ugumu wa kupatikana kwa vifaa vya ujenzi kama seruji na mafundi ambao wangewezesha kukamilisha ujenzi huo kwa wakati hivyo wameahidi ujenzi utakamilika ifikapo Machi 2025.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa