Kamati ya lishe wilaya ya Ikungi yagawa mbegu za mbogamboga kwa watendaji ili kuonyesha mfano kwa jamii zinazowazunguka haswa mashuleni .Katika kikao hicho cha maafisa wa afya ,kamati tendaji ya lishe na watendaji wa kata,wamejadili mambo ya lishe,utendaji kazi kama timu kwaajili ya kuimarisha afya za jamii pamoja na mashuleni kwa kuzingatia mlo kamiliPia katika kikao hicho Mratibu wa m -mama tuwavushe,amesema kwamba maafisa afya na watendaji waendelee kuepusha vifo vya watoto na mama kwa kuwa na ushirikiano katika kufanya kazi.Pia kaimu mkurugenzi mtendaji ndg Eva myula amesisitiza watendaji kulete ripoti za lishe mashuleni kwa wakati na watu wa afya wapunguze mimba za utotoni katika jamii kwa kutoka elimu ya madhara ya mimba hizo.Mwisho kikao hicho kimeazimia kufikia robo ya Kwanza ziwe kijani kwenye kata zote.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa