Kamati ya Pembejeo wakishirikiana na kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikungi wajadili namna nzuri itakayowezesha usambazaji wa mbolea na mbegu katika vijiji vyote Wilaya ya Ikungi.Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya hii Mhe Thomas Apson amesema kuwa Mkoa wa Singida umefikia asilimia 83 ya utumiaji wa mbolea na unategemea kuongeza uzalishaji msimu huu wa kilimo"Lengo letu ni kuboresha kilimo Mkoa wa Singida Wilaya ya Ikungi kwa kutumia mbolea na viuwatilifu kufikia kilimo chenye tija"Amesema ApsonSerikali imelipia asilimia 50 ya mbegu na mbolea ili kuwapa unafuu wakulima kufikia adhima ya kilimo bora na Wilaya imepewa jukumu la kuhakikisha mbolea inafika kwa wananchi wa vijiji vyote Wilayani Ikungi.Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo amesema kuwa baadhi ya kata ambazo hazijafikiwa na mbegu pamoja na mbolea ni kata ya Misugaa,Kikio, minyughe,Ighombwe Mtunduru na zingine kadhaa na kuanzia wiki hii wananchi watapata mbegu hizo kwani tayari Ikungi imepokea Tani 23 Za mbegu siku ya Uzinduzi wa usambazaji wa mbegu Mkoani Singida.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa