Kamati ya siasa Wilaya ya Ikungi ikiongozwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya Dr. Mika Tano Likapakapa yatembelea miradi mbalimbali na kupongeza juhudi za usimamiaji miradi hiyo ili iweze kuwanufaisha wananchi katika wilaya yetu.
Katika ziara hiyo ya siku mbili mfululizo kamati imepitia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja Kijiji cha Minyughe linalogharimu kiasi cha milioni 250.3, ujenzi wa shule tatu mpya za sekondari samamba, kitandaa na kinku ambazo kila shule inagharimu milioni 544, mradi wa ujenzi tanki la maji kijiji cha Munyu unaogharimu milioni 390 na unaenda kuhudumia takribani wakazi 2199, mradi wa CSR ujenzi wa vyumba vya maduka stendi mpya Ikungi na ujenzi wa vyumba vya maduka manispaa ya singida ambapo miradi mingi ipo hatua za ukamilishaji.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 08 Aprili, 2025 hadi 09 aprili, 2025 lengo ni kuhakikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa kwa ujenzi wa miradi bora na inayokamilika kwa wakati.
Baadhi ya viongozi wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM Wilaya wamepongeza ubora wa miradi hiyo na kusisitiza iweze kukamilika kwa wakati ili ianze kutoa huduma wananchi katika maeneo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa