Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Ikungi yashauri kutoa huduma za lishe mashuleni ili kutengeneza afya za wanafunzi kuleta matokeo bora katika ujifunzaji.
Kikao hicho maalumu cha kamati ya ushauri ya wilaya ya ikungi DDC kimefanyika tarehe 10 februari 2023 katika ukumbi wa halamashauri ya wilaya ya Ikungi na kujadili kuhusu rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo moja ya ushauri uliotolewa ni pamoja na kuweka utaratibu wa lishe mashuleni ili watoto wapate afya bora kwa ajili ya mstakabali wa masomo yao na hatimaye kuongezeka kwa ufaulu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson ndiye alikua mwenyekiti wa kikao hicho maalumu ambapo ajenda kuu ilikuwa kupitia ana kujadili bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi disemba 2022/2023,makisio ya ya rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024, lakini pia kamati ilipitia na makisio ya rasimu ya mpango wa bajeti ya TARURA na RUWASA kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Aidha katika mwaka wa fedha 2023/2024 halmashauri ya wilaya aya Ikungi imekisia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi za kitanzania zaidi ya Bilioni 39.2,kwa upande wa TARURA wamekisia shilingi za kitanzania bilioni zaidi 4.4 lakini RUWASA ni shilingi za kitanzania zaidi ya bilioni 2.3.
Pamoja na hayo mkuu wa wilaya aliwaomba viongozi kushirikiana na wanachi katika kuleta maendeleo wilaya ya Ikungi na ameagiza taarifa katika kila miradi ya Ikungi kuandaliwa kwa ajili ya ziara ya kutembelea miradi yote iliopo Wilayani hapa inayokuja hivi karibuni.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa