Afisa elimu msingi na awali Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Margaret Kapolesya afungua mafunzo ya siku tano kuwawezesha walimu wa darasa la kwanza kutumia mbinu stahiki za ufundishaji na ujifunzaji wa unahiri wa Kiingereza na KKK kwa kuzingatia mtaala ulioboreshwa mwaka 2023.
Akizungumza na walimu kabla ya kufungua mafunzo hayo leo tarehe 12 mwezi Februari 2023 amesema baada ya mafunzo haya walimu walioshiriki watahitajika kwenda kufanya uwezeshaji katika jumuiya za kujifunza (JzK) ili walimu wengine waweze kuongeza umahiri katika ufundishaji wa lugha ya Kiingereza, Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa kutumia mbinu jumuishi.
"Mabadiliko makubwa yamefanyika katika mitaala mipya ili kufanikisha utekelezaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa umahiri wa Kiingereza, kusoma, kuandika na kuhesabu, na (TET) imeandaa mafunzo endelevu kwa walimu kazini kuhusu utekelezaji wa mitaala ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji hivyo tuwape ushirikiano wakutosha wawezeshaji ili tuweze kuwa msaada Kwa watoto wetu", amezungumza Kapolesya
Morice Mkhotya ni Mratibu wa mafunzo kutoka wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema kuwa mafunzo haya yatawafikia walimu 639 wanaofundisha darasa la kwanza katika shule zote za msingi zilizopo mkoani Singida kuanzia tarehe 12/02/2024 hadi 16/02/2024 mwaka 2024.
Mratibu huyo ameongeza na kusema kuwa maeneo yatakayowezeshwa katika mafunzo hayo ni pamoja na kufanya tathmini ya ufundishaji na ujifunzaji kulingana na mtaala ulioboreshwa 2023, ufundishaji wa matamshi ya sauti za herufi za Kiswahili na Kiingereza LAT, kona za ujifunzaji, uboreshaji na utekelezaji wa mchakato wa maandalizi ya ufundishaji na ujifunzaji, TEHAMA na Teknolojia saidizi,ushairi na unasihi, uhuishaji wa mpangokazi wa utekelekezaji wa mafunzo katika JzK na mengine yanayomjenga kwa haraka mtoto.
"Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imekamilisha kazi ya kuandaa mitaala na mihtasari ya masomo yote kwa Elimu msingi, Sekondari ya Juu na Ualimu hivyo ni jukumu letu kwenda na kasi ya mtaala mpya kuwasaidia wanafunzi kufikia ndoto zao",amesema mratibu wa mafunzo hayo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa