Karibu Tawala Wilaya ya Ikungi Mhe. Rashid M.Rashid azindua chanjo ya HPV (Human Papilloma Virus) saratani ya mlango wa kizazi inayotarajiwa kuanza katika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida Tarehe 22 hadi 26 Aprili 2024.Katika uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Tarehe 19 Aprili 2024 katibu tawala amesema kuwa kampeni ya chanjo hiyo inalenga kuwafikia zaidi ya wasichana elfu 37.7 wenye umri kati ya miaka 9 hadi miaka 14.Kaimu Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi-Haika Massawe ameongeza na kusema atakuwa tayari kushirikiana kwa karibu na timu itakayoendesha zoezi hilo ikiwa ni pamoja na idara ya elimu msingi na sekondari pamoja na watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha tunawachanja wasichana wote walio shule na wasio shuleni katika wilaya yetu.Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Bi-Oliva Njoka amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya kuchelewa Kwa fedha za kampeni kufika ngazi ya Halmashauri, ufinyu wa bajeti pamoja na baadhi ya taasisi za shule za dini kutokuruhusu wasichana wanaoishi bwenini kupata chanjo bila idhini ya wazazi wao hivyo kupelekea kutokufikia malengo."Kuna haja ya kuendelea kuwapa elimu wananchi juu ya faidi za hii chanjo kwa watoto wa kike wenye umri lengwa" amezungumza Mganga mkuu
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa