Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Ikungi kwa kusimamia miradi mbalimbali inayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan...Akizungumza mara baada ya kutembea hospital ya Wilaya ya Ikungi iliyogharimu takribani bilioni 1.9 katibu mkuu amesema kuwa hospital imejengwa kwa kiwango kinachoridhisha na kuanza kutumika kwa wakati."nawapongeza uongozi wa hospital, Halmashauri ya wilaya kwani licha ya upungufu wa vifaa mmeona vyema kuanza kutoa huduma nawapongeza sana" alisema Chongolo.Kwa upande mwingine Katibu mkuu amepongeza utunzaji wa mazingira katika hospital kwa kupanda miti mbalimbali ambayo itasaidia kupata sehemu za vivuli na matunda.Ziara hiyo imeanzia kata ya Mkiwa kijiji cha choda ambacho kipo mpakani mwa Wilaya ya Manyoni na Ikungi na katibu alitembelea mashamba ya wawekezaji, alifika shina namba 11 kijiji cha Ulyampiti baadae alitembelea Veta, Hospital ya Wilaya,Shanta Gold Mine, Sekondari ya Puma na Ikungi badae alimalizia kwa Kufungua Ofisi ya CCM Wilaya na kuzungumza na wananchi.Aidha Katibu mkuu amewaomba wananchi kushirikiana vyema na wananchi ili kukuza maendeleo Wilayani hapa lakini pia aliwataka viongozi kujenga tabia ya kuwafikia wananchi wote hadi wale waliopo vijijini.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa