Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Peter Serukamba asikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Ikungi na kutatua baadhi ya kero akishirikiana na viongozi mbalimbali akiwepo mkuu wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, na idara za Halmashauri ya Wilaya hiyo...Akizungumza na wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao Viwanja vya Soko la mbona mboga Kijiji cha Ikungi tarehe 23 Februari 2023 Mkuu wa mkoa amesema kuwa wananchi wawe wanashirikiana kwa karibu na viongozi wa halmashauri ili kutatua kero zao na sio kusubiri mpaka mkuu wa mkoa aje kuwasikiliza...Awali wakiuliza maswali wananchi wengi wamekuwa na migogoro ya aridhi ambayo Afisa ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Ambrose Ngonyani ameahidi kuitatua ifikapo Jumatano ya wiki ijayo ambapo aliwatangazia wote wenye migogoro ya ardhi juma tatu ya wiki ijayo waende ofisi ya ardhi wilayani hapa kusikilizwa na kuona jinsi ya kutatua migogoro hiyo ya ardhi...Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg Richard Rwehumbiza amewaomba wananchi wawe wavumilivu pale migogoro ya ardhi inapotokea na kufata taratibu za kisheria na sio kujichukulia ardhi au hatua bila kufata taratibu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa