Kamati ya lishe wilaya ya ikungi hapo jana tarehe 18 julai 2023,amekaa na kujadili lishe mashuleni na kwa jamii nzima.Katika kikao hicho ndg mkurugenzi mtendaji Justice L Kijazi wa wilaya hiyo ,amesema kuwa mbali na kusisitiza kuwa elimu ya lishe itolewe kwa jamii,aliwaomba Viongozi wa dini walau watoe dakika Tano na wazungumzie kuhusu lishe kwa waumini kwani kiwango kikubwa cha jamii kinapatikana kwenye nyumba za ibada.Pia katika kikao hicho mratibu wa lishe ,ndg Nevu Dickson amesema kuwa wababa wawe chachu ya kuelimisha familia zao kuhusu swala la lishe,idara mtambuka kuendelea kutoka elimu juu ya lishe kwa kata zote za wilaya ya ikungi na wazee wawe mstari wa mbele kuelimisha jamiiPia Afisa elimu msingi ndg Magareth kapolyesia amesema kuwa tayari wameshaanza kutunza bustani mashuleni zitakazo dumu mwaka mzima kwa njia ya umwagiliaji.Katika kamati hiyo mjumbe mmoja ndg amesisitiza wanakamati kutembelea mashuleni ili nao kuweze kutoka msisitizo kwa wazazi kuhusu lishe .Mwisho kiongozi wa dini ndg Joyce amechangia kwa kusema"uzuri wa vyakula vya mlo kamili vinapatikana hapa hapa wilayani sio nje ya nchi,kwahiyo ili jambo linawezekana kwa jamii zetu".
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa