Katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson, juzi tarehe 22 Novemba 2023, kata ya Misughaa na kata ya Kikio amewataka wananchi kutunza misitu ili kuingiza kipato kupitia hewa ya ukaa na hatimaye kukuza maendeleo katika wilaya ya Ikungi.Mhe. Apson ametembelea madaraja ya kijiji cha Msule yanayojengwa na TARURA, zahanati ya Msule iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kumaliziwa na serikali kwa shilingi milioni 50. Mkuu wa Wilaya huyo pia alitembelea shule za msingi za vijiji vya Msule na Sakaa kuona upungufu wa majengo ya madarasa, nyumba za walimu na upungufu wa vyoo vya shule hizo kabla hajaongea na wananchi na kusikiliza kero zao katika kijiji cha Sakaa.Kero kubwa ambazo zimezungumzwa na wananchi hao ni pamoja na maji, nishati ya umeme, uhaba wa nyumba za watumishi katika idara zote ndani ya kata ya Misughaa.Wakati akijibu maswali ya Wananchi amesema kuwa amepokea kuwepo kwa tatizo la maji katika kata ya Misughaa na atalipeleka kwa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi huo unaoendelea kwani upo katika hatua za umaliziaji.Mhe. Apson pia ametembelea kata ya Kikio na kukagua ujenzi wa Nyumba mbili za walimu. Katika nyumba hizo moja iko katika hatua za ukamilishaji ambayo inagharimu takribani Milioni 29 na jengo la pili linajengwa kwa nguvu za wananchi na ujenzi wake upo katika hatua ya usawa wa madirisha.Mara baada ya ukaguzi huo alizungumza na wananchi wa kata ya Kikio, kijiji cha Mnane ambapo kero kubwa zaidi zilizobainika ni kuwepo kwa unyanyasaji wa kijinsia, ukosefu wa mbegu za mazao mbalimbali kama alizeti na mahindi; mbolea, ukosefu wa maji na kadhalika.MWISHOImetolewa na;Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi24 November 2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa