Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Ndg Rashid M.Rashid aongozo zoezi la upandaji miti katika shule ya Msingi Kipumbwiko akishirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Kijazi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson Akisoma taarifa hiyo Bwana Legan Elfoni Afisa Misitu wilaya ya Ikungi amesema kuwa wilaya ya Ikungi inatarajia kupanda jumla ya miche 1,500,000 katika maeneo mbalimbali ambapo mpaka kufikia tarehe 14/02/2024 jumla ya miche ya miti 127,571 imesambazwa na kupandwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Ikungi na zoezi la usambazaji wa miche linaendelea Ameongeza na kusema kuwa miche ya miti iliyosambazwa na kupandwa ni pamoja na miti ya matunda, mbao, na kivuli na leo katika zoezi hili miche ipatayo 1,000 katika maeneo ya umma, taasisi pamoja na maeneo ya watu binafsi itapandwa."tunapenda kukushukuru tena Mhe Mgeni Rasmi viongozi na wananchi wote mliofika katika maadhimisho haya ya kilele cha upandaji miti kwa msimu wa mwaka 2024 hivyo ni jukumu letu kwa ujumla kusimamia na kuitunza miti iliyopandwa kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho"amesema Afisa Misitu.Kwa upande wake mgeni Rasmi katika zoezi hilo amesema mwamko wa upandaji miti katika wilaya yetu unazidi kuimarika mwaka hadi mwaka kutokana na wananchi kupata elimu ya kuhifadhi mazingira kwa njia ya kupanda miti ya aina mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira."Nitoe rai kwa viongozi wote tuzidi kutoa elimu kwa wananchi na wanafunzi juu ya umuhimu wa upandaji miti na uhifadhi wa mazingira kwa mustakabali wa maisha yetu kwani miti ni uhai",amezunguza DASAidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi ametoa shukrani za dhati na kulipongeza Shirika lisilo la Kiserikali la Trees For The Future kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kufanikisha zoezi zima la kuandaa kitalu cha miche katika kijiji cha Mungaa ambapo sehemu kubwa ya miche inayopandwa msimu huu inatokana na kitalu hicho.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa