Mkaguzi wa ndani halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg Philemon Daftari amewatembelea wakulima wa vikundi ya mradi wa UN women wanaojihusisha na kilimo umwagiliaji cha mahindi,vitunguu,nyanya na pilipili…
Mkaguzi huyo amewatembelea wakulima tarehe 19 septemba,2022 ambao wanajishughulisha na kilimo cha umwgiliaji wilaya ya Ikungi katika kata tatu Ambazo ni kata ya Dumunyi,Irisya,na Sepuka na ndani ya kata hizo kuna vijiji vinne ambavyo vinajihusisha na kilimo hicho ambavyo ni pamoja na kijiji cha Kipumbuiko,Mnaghana,Munyu na Irisya…
Daftari aliwashauri viongozi wa wakulima juu ya kilimo bora na chenye tija na kuwasikiliza wataalamu wa maswala ya kilimo juu ya matumizi mazuri ya viwatilifu ili kupata mazao bora…
Sera ya vikundi vya mradi wa UN Women ni tufikie usawa kumwezesha mwanamke na msichana.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa