Kikao kazi cha uhabarisho na tathimini ya zoezi la ugawaji wa dawa za kichocho na minyoo ya tumbo kwa watoto wenye umri kuanzia miaka mitano (5) hadi kumi na nne (14) kufunguliwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Ndg. Edward Mpogolo.Kikao hicho kilihudhuriwa na Watendaji wa Halmashauri Idara ya Afya, na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo. Aidha alisisitiza kuwa zoezi hili lifanyike kwa kuzingatia taratibu za Afya ikiwemo wanafunzi kupewa chakula kabla ya kumeza dawa na aliahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika zoezi hili kwa kuwashirikisha viongozi wa serlkali wakiwemo Madiwani , watendaji wa Kata,watendaji wa vijiji na wenyeviti wa kijiji ili kufanikisha zoezi hili kwa ufasaha na hasa katika kuchangia chakula cha wanafunzi ili kuepusha kupata madhara yatokanayo na kumeza dawa bila kula.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri Ndg. Ally Mwanga na Mkurugenzi Mtendaji Ndg, Justice Kijazi walimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuonesha ushirikiano katika zoezi hili muhimu na jinsi anavyojitoa kushiriki katika kazi za jamii.
Habari picha
Washiriki wa Kikao cha Uhabarisho na Tathimini ya zoezi la ugawaji wa dawa za kichocho na minyoo wakitafakari kwa makini umuhimu wa zoezi hili
Mwenyekiti wa Halmashauri akisisitiza umuhimu wa kingatiba ya kichocho na minyoo tumbo kwa watoto wenye umri kuanzia miaka mitano (5) hadi kumi na nne (14).
Mkurugenzi Mtendaji akiwasisitiza watendaji wa Afya kufanya kazi kwa kufuata taratibu za Afya na kuwaasa kuwa zoezi hili lifanyike kwa kuzingatia muda uliotelewa na asiwepo mlengwa yeyote atakayekosa dawa hizi muhimu.
Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Bi. Lucina Kimaro akitoa tathimini ya zoezi zima la kugawa kingatiba kwa watoto. Alisema zoezi hili limesaidia sana kupunguza kasi ya maambukizi ya magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo. Ameahidi kusimamia zoezi hili kwa ufanisi mkubwa.
Mkuu wa Wilaya akisikiliza kwa makini Taarifa iliyosomwa na Mratibu wa magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo.
Kaimu Mgaga Mkuu wa Wilaya (pichani akiandika) Ndg. Philipo Kitundu akichukua nukuu za mambo muhimu yaliyozungumzwa katika kikao hicho. Pichani ni washiriki wa kikao hicho akiwemo Afisa Elimu Sekondari, Kaimu mweka Hazina na Afisa Manunuzi.
Matukio katika Picha
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa