Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndg. Ismail Ussi, ametembelea na kukagua Mradi wa Uchomeleaji na Utengenezaji wa Vifaa vya Aluminium unaotekelezwa na Kikundi cha vijana cha Boys Ikungi kilichopo katika Kata ya Ikungi, Kijiji cha Ikungi.
Kikundi hicho kilianzishwa tarehe 23 Juni 2022 na kimesajiliwa rasmi katika mfumo wa Nest kwa namba SIN/IKU/VIJ/2023/0021, kikiwa na wanachama watano (5) wote wanaume. Mradi huo unagharimu shilingi milioni 10.4, ambapo shilingi milioni 10 ni mkopo kutoka asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, huku mashine moja ya kuchomelea yenye thamani ya shilingi 400,000 ikitolewa kwa msaada kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mradi huo unalenga kutoa ajira kwa vijana, kuwapa ujuzi wa uchomeleaji na utengenezaji wa bidhaa za aluminium, pamoja na kuhudumia wananchi kwa bidhaa bora. Hadi sasa, vijana 10 wamepata mafunzo kupitia mradi huo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi, Mwenyekiti wa kikundi, Ridhiwani Mussa Shabani, alieleza matarajio ya mradi kuwa ni kuongeza uzalishaji wa bidhaa bora, kupanua soko la bidhaa ndani na nje ya wilaya, na kutoa ajira zaidi kwa vijana.
Mwenge wa Uhuru 2025 umebeba kaulimbiu isemayo: “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.”
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa