Wananchi kata Ntuntu wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wameishukuru serikali kwa kuwajengea kituo cha afya kitakachowasaidia wananchi hao kuifikia huduma kwa urahisi...
Kituo hicho cha afya kiliyotembelewa na Mkurugenzi wa huduma za Afya lishe na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) Dkt. Ntuli Kapologwe pamoja na timu yake kutoka ofisi hiyo wakiongozana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida na Timu yake (RHMT) kujionea hatua mbalimbali za ujenzi wa Kituo hicho hivi karibuni na sasa imeanza kutumika rasmi tarehe 28 Novemba 2022.
Mkurugenzi huyu pamoja na timu yake amepongeza Timu ya usimamizi wa ujenzi wa Kituo hicho cha Afya kwa ukamilishaji mzuri wa majengo 3 ya awamu ya kwanza (Jengo la Wagonjwa wa Nje OPD, Jengo la Maabara na Kichomea Taka) kwa kukamilika kwa asilimia 99% na kutoa maelekezo sasa Wananchi waanze kupata huduma kuanzi Jumatatu ya Tarehe 28/11/2022 na kueleza kuwa Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za uletaji wa vifaa tiba mbalimbali katika Kituo hicho.
Aidha Katika majengo 3 ya awamu 2 (Jengo la Wodi ya Wazazi (Maternity), Jengo la Upasuaji (Theatre) na Jengo la Kufulia (Laundry) Mkurugenzi huyu kutoka (Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) pia amekagua na kupongeza kwa hatua za Majengo hayo ilipofika na kusema Majengo yamefikia zaidi ya asilimia 60% hivyo ametoa maelekezo kuwa Kasi ya ujenzi iongezeke hadi kufikia Disemba 30 Majengo hayo yawe yamekamilika ili kufikia malengo ya Serikali ya kupeleka huduma kwa wananchi wa Ikungi hasa kata ya Ntuntu.
Aidha Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Dkt Michael Solomon pamoja na viongozi wa kijiji hicho wamefika kituoni hapo kujionea hali halisi ya maendeleo ya kiyuo hicho cha afya baada ya kuanza kutumika mapema hii leo na kusema kuwa wananchi wanapaswa kutunza mazingira ya kituo hicho ikiwepo vyoo na manzingira yote ya nje na ndani ya kituo hicho cha afya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa