Kliniki ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi yaendelea ambapo baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi wamejitokeza kwa ajili ya kushughulikiwa kero zao.
Hayo yamefanyika hii leo tarehe 11 Julai, 2024 katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ambapo kero kubwa imekuwa ni tatizo la ardhi ambapo Mkuu wa Wilaya, idara ya ardhi wakishirikiana na mwanasheria wamepata nafasi ya kuwasikiliza wenye migogoro hiyo ya ardhi na kutoa maamuzi yenye msaada sawa pande zote.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson amezungumza na wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kabla ya kuanza kwa zoezi hilo na kuwaambia kuwa kliniki hii imekua msaada kwa wananchi kwani wamejitahidi kutatua kero nyingi kwa kipindi kufupi.
"Tulivyoanza tuliona idadi kubwa sana ya watu wakifika hapa na kero zao mbalimbali ila mpaka sasa kama tunavyoona watu waliokuja leo kuleta kero zao ni wachache sana ukilinganisha na mwanzo hivyo hii inaonyesha wazi tumefanikiwa kufikia lengo na maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Halima Dendego" amezungumza DC.Thomas Apson.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa zoezi hili ni endelevu na lengo ni kuwafikia wananchi wengi zaidi kadri muda utakavyoenda kwani ndio njia rahisi kuwapata wananchi wengi zaidi.
Uziduzi wa kliniki ya kushughulikia kero za wananchi wa Wilaya ya Ikungi ulifanyika tarehe 13 Juni, 2024 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Mhe Rashid M. Rashid akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Thomas Apson aliongoza zoezi hilo la uzinduzi kuhakikisha adhima ya zoezi hilo inatimia.
Naye kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Singida mashariki Mhe Miraji Mtaturu amempongeza Mkuu wa mkoa wa Singida, Mkuu wa wilaya ya Ikungi pamoja na wakuu wa idara na vitengo kwa kutenga siku ya alhamisi katika kila juma kusikiliza kero za wananchi na kuwaomba waendelee na moyo huo
MWISHO.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa