Mkuu wa divisheni ya Utumishi Bi-Edna Palla akiongozana na maafisa utumishi wengine awataka watumishi wa umma kuzingatia sheria taratibu na miongozo ili kutimiza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kikamilifu.
Hayo yamesemwa katika ziara yake hii leo tarehe 13 Juni, 2025 alipokuwa akisikiliza na kushughulikia kero za watumishi katika kata ya Iyumbu ambapo watumishi mbalimbali kutoka sekta ya afya, kilimo, elimu na maendeleo ya jamii wamezungumza na maafisa utumishi kujadili wajibu wao kuhakikisha wananchi wanapata manufaa kupitia utendaji wao wa kazi.
Afisa Utumishi amesema kuwa baadhi ya watumishi umma hawazingatii taratibu za kiutumishi kama vile mahudhurio kazini, kutokuomba ruhusa wanapopata dharura, kutokutunza mali za umma hali inayopelekea watumishi hao kushindwa kutimiza majukumu ya kazi kikamilifu.
"Kutokutimiza majukumu yako vyema katika kazi ni sawa na mwizi kwani unaiba muda wa serikali na kufanya mambo yako binafsi, kuna haja yakubadilika serikali imetuamini" amesisitiza kwa mifano Afisa Utumushi.
Kwa upande wao baadhi ya watumishi wameeleza changamoto zao kuwa ni pamoja na kuchelewa kwa malipo ya likizo, upandaji wa madaraja, na changamoto ya mfumo wa kujaza majukumu ya watumishi PEPMIS na maafisa hao wametoa majibu na kutatua baadhi ya changamoto zao huku wakisisitiza kutoa taarifa kwa viongozi husika ili changamoto hizo ziweze kutatuliwa kwa wakati.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa