Maafisa kilimo,Wakulima ,wanunuzi ,Wasindikaji na wauzaji wa pembejeo wapata elimu ya fedha kutoka AFDP(Agriculture and Fishering Development Program).Mafunzo hayo yameshirikisha maafisa kutoka wizara ya kilimo na banki ya kilimo(TADB) katika utekelezaji wa mafunzo ya elimu ya fedha .Lengo la elimu ya fedha kwa wadau ni kuwawezesha, kuongeza uwekezaji katika kilimo ,kujadili mbinu mbalimbali za kufikia vyanzo vya fedha , matumizi sahihi ya rasilimali fedha,utoshelevu wa chakula nchini na kuleta mapinduzi ya kilimo.Katika mafunzo hayo Ndg Ernest Kibulei kutoka Wizara ya kilimo amewaambia wadau waendelee kulima mazao ya Alizeti,Mahindi na jamii ya mikunde kwa kutumia mbegu bora,mbolea za kisasa za kupandia na kukuzia kwa lengo la kuzalisha kwa wingi ili tujilishe,tuwalishe na tuuze nje ya nchi .Pia katika mafunzo hayo Ndg Chrisker Masaki kutoka Banki ya kilimo (TADB)amesisitiza wadau kuchukua mkopo kwa ajili ya kilimo lakini sio wakope kwa biashara inayoanza,pia amesisistiza wadau kabla ya kukopa panga kwanza ,weka kumbukumbu za fedha,ulipanda lini ,ulipalilia lini na kuvuna.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa