Afisa maendeleo ya jamii Bi Haika Massawe awataka maafisa maendeleo katika kila kata kutimiza majukumu yao kama walivyojaza kwenye barua zao za ajira ili kuhakilisha wananchi wanapata huduma zote zinazostahili kutoka kwao.Hayo yamesemwa katika kikao cha maafisa maendeleo kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ambapo mkuu wa idara hiyo amezungumza nao juu ya maadili kazini na kutimiza majukumu yao lengo ikiwa ni kuwafanya waongeze ufanisi kazini.Hata hivyo kikao hicho kiliambatana na mafunzo ya mfumo wa WEZESHA PORTAL ambapo Afisa biashara pamoja na Afisa Maendeleo Ndg.Peter Nchimbi wametoa maelekezo ya namna ya kujisajili katika mfumo huo utakao wawezesha walengwa kujisajili katika mikopo ya asilimia 10 za halmashauri.Hata hivyo baadhi ya maafisa maendeleo wa kata wamepongeza idara ya maendeleo ya jamii kwa kutoa mafunzo hayo kwani matumizi ya mfumo huo yanaenda kutoa adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu ndipo wasajili vikundi badala yake WEZESHA PORTAL imekua shuluhisho katika adha hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa