Maafisa masuuli waelekezwa kuanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa ununuzi wa umma NeST katika michakato yote ya ununuzi wa umma.Hayo yamesemwa leo tarehe 13 Januari, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice Kijazi katika mafunzo ya mfumo huo yanayofanyika kwa siku mbili ukumbi wa Halmshauri ya Ikungi.Mkurugenzi ameongeza na kusema kuwa watumishi wote wanaohusika na mchakato wa ununuzi ndani ya taasisi wanapaswa kupata mafunzo yatakayomuwezesha kutumia mfumo huo wa manunuzi kwa ufasaha ili kuepusha ubadhilifu wa fedha za serikali."Wanaopaswa kushiriki mafunzo hayo ni pamoja na maafisa masuhuli, wakuu wa idara na vitengo, maafisa wawili kwa kila idara au kitengo wanaohusika na manunuzi, mkaguzi wa ndani, maafisa tehama na mwanasheria wa taasisi." amezungumza KijaziKwa upande wake Mkuu wa Idara ya manunuzi Wilaya ya Ikungi Bi Mariam A. Haroun amesema kwa mujibu wa kifungu Cha 9 (1)(k) cha sheria ya ununuzi wa umma, sura ya 410, mamlaka ya kudhibiti wa ununuzi wa umma PPRA imekasimiwa jukumu la kusanifu, kuanzisha na kuhuisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki kwa ajili ya uwazi na kuleta tija kwenye ununuzi wa umma."Hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kujifunza mfumo wa NeST na kujisajili ili kurahisisha huduma za manunuzi kwa njia ya mtandao" anasema Bi Mariam Hata hivyo kwa upande wao baadhi ya watumishi waliopata mafunzo hayo yamesema kuwa mafunzo hayo yanaenda kuwa muarobaini wa upotevu wa fedha za serikali kwani kila manunuzi yanaenda kufanyika kwa njia ya mtandao NeST na wapo tayari kujisajili na kuanza kutumia mfumo huu rasmi@ikulu_mawasiliano@teamsamia_suluhu@samia_suluhu_hassan@ortamisemi@urtmof@dr_philip_isdor_mpango
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa