Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg Justice aongoza zoezi la ugawaji wa simu janja 6 kwa wakulima 6 wanawake na tablet 3 kwa maafisa ugani kutoka kata za Dungunyi , Sepuka na Irisya tumepokea kutoka Farm Africa chini ya ufadhili wa Un Women...
Akizungumza mara baada ya kugawa simu hizo kwa walengwa tarehe 19 Januari 2023 mkurugenzi amesema kuwa lengo la kugawa simu hizo ni kusaidia kukusanya Takwimu ,Kutunza na kupata taarifa za Masoko ya Mazao wanayozalisha katika maeneo yao...
Kijazi ameongeza na kusema kuwa simu hizo zitumike pekee kwa lengo lililokusudiwa na sio vinginevyo ili kukuza kilimo katika wilaya yetu...
Kwa upande Wake Afisa Kilimo Gurisha Msemo amesisitiza kuwa kutumia vizuri msimu wa mvua hizi za wastani kupanda mazao ya muda mfupi ili kuepukana na njaa na Umasikini.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa