Kitengo cha manunuzi pamoja na idara ya elimu sekondari yafanya kikao kazi na wakuu wa shule na wahasibu juu ya maelekezo na mafunzo ya mfumo wa manunuzi NEST kupitia mtandao.
Mafunzo hayo yametolewa leo tarehe 21 Octoba, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri na Afisa Manunuzi Bi Mariam Haroun pamoja na Bi Mercy Ringo ambaye anashughulikia Idara ya Elimu sekondari kwa upande wa manunuzi.
Bi Mariam amewataka walimu kueleza changamoto wanazopitia wakati wa utekelezaji wa manunuzi kupitia mfumo wa manunuzi mtandaoni NEST.
"Tukumbuke kwamba mfumo wa manunuzi serikalini kupitia mtandao ulizinduliwa tarehe 09 Septemba, 2024 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kurahisisha huduma ya manunuzi hivyo tuendelee kujifunza zaidi" amesema Bi Mariam
Kwa upande wao walimu wakuu na wahasibu wameeleza changamoto zao wanazopitia Katika mfumo huo wa manunuzi na kuzijadili kwa kina ili kuhakikisha changamoto zao zinatatuliwa kwa wakati.
"Hivyo ni rai yetu kama taasisi kuhakikisha hakuna manunuzi yeyote yanafanyika bila mfumo huu rasmi wa manunuzi" Amezungumza Afisa Manunuzi.
Kwa upande wake Afisa elimu sekondari Ndg Ngwano J. Ngwano amewasisitiza walimu wa fedha na wakuu wa shule kuhakikisha wanafuata maelekezo yote yaliyotolewa pia amewaambia kua hakuna pesa yoyote ile itaongezwa kwenye fedha za miradi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa