Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Ikungi ikiongozwa na Bi Haika Massawe Mkuu wa Divisheni washirikisha wananchi na wataalam wa Kata ya Puma kutoa mawazo yatakayosaidia kutengeneza vipeperushi na mabango yenye ujumbe wa kuhamasisha usawa wa kijinsia katika jamii inayotuzunguka.Akizungumza Tarehe 13 Novemba,2023 kabla na baada ya kupokea maoni hayo Bi Haika amesema kuwa lengo la uchapishaji wa nakala hizo ni kuwapa uelewa jamii kupunguza ukatili wa kijinsia,Uwezeshaji Wanawake kiuchumi,Mgawanyo wa Majukumu katika familia,Kuthamini kazi za huduma na matunzo zifanywazo na Wanawake na Wasichana na njia muhimu za kimpunguzia mwanamke mzigo wa kazi zisizo na malipo majumbani ikiwa ni mchakato wa kuweza kusaidia kuongeza kasi ya uwezeshaji wa mwanamke wa kijijini kiuchumi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa