Afisa mazingira wa kampuni ya uchimbaji shanta Ndg Mkisi ametoa mafunzo kwa wananchi wa kijiji cha
Matare kuhusu kemikali ya sumu itakayo pita kutokea Daresalaam kuelekea kwenye mgodi wa Shanta uliyoko Mang'onyi wilaya ya ikungi hapo jana tarehe 24 januari 2023.
katika mafunzo hayo Wananchi pamoja na watoto wameelimishwa kuhusu kemikali hiyo ambayo ni sumu kwa wanadamu pamoja na wanyama .alieleza kuwa sumu hiyo endapo itashikana na maji itatoa hewa ambayo itasababisha maafa eneo husika .
Afisa huyu amesema kuwa wananchi wachukue tahadhali wakati magari hayo yakipita kuelekea kwenye kampuni ya madini.endapo magari hayo yakidondosha au kupata ajali wakae mbali nayo kwa usalama zaidi.
Amesisistiza kuwa magari hayo yamewekwa alama ya kitambaa chekundu chenye neno Hatari.kwa kumaanisha kilichobebwa si salama.
katika mkutano huo wamewahasa wanafunzi kutoa taarifa kwa wazazi ambao hawakuweza kufika eneo la mkutano kutoa taarifa kwa wazazi na pamoja na ndugu na jamaa wakaribu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa