Balozi wa zao la Pamba nchini Ndg Agrey Mwanri Aendelea kutoa Mafungo ya kilimo cha Pamba katika Mkoa wa Singida wilayani Ikungi...
Mafunzo hayo yamendelea katika Kijiji cha Sambaru na vijiji vingine wilaya ya Ikungi tangu yalipofanyiwa uzinduzi katika ukumbi wa halmashauri ya Ikungi Tarehe 6 Octoba.
Agrey amewahakikishia wakulima kuwa endapo watalima kwa kufata taratibu za kilimo cha zao hilo wataondokana na umasikini. "Zao la Pamba linahitajika sana na nchi mbalimbali Duniani hivyo biashara yake sio ya kubahatisha Limeni sana ili tujikwamie kiuchumi."
Kwa upande wake Mweyekiti kamati ya Huduma za Uchumi halmashauri ya wilaya ya Ikungi aliongeza na kusema Msimu wa kilimo 2022/2023 tuhakikise tunalima kwa wingi ili kuwapa hamasa watoa Mafunzo juu ya kilichofundishwa na utekulezaji wake.
Pia aliwapongeza wakulima kwa kujitokeza kwa wingi katika Mafunzo hayo na kuwashukuru endapo Mafunzo hayo yataleta matokeo chanya katika wilaya hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa