Mwezeshaji wa Semina Bwana. Vitus Kakonko ambaye Pia ni Mhasibu wa Tamisemi akiendesha Mafunzo ya Semina ya Mkoani Dodoma Kuhusu Mfumo wa ukusanyaji Mapato kwa njia ya kielekroniki katika mamlaka za Serikali za Mitaa (LGRCIS) kwa Maafisa Tehama, Mafisa Biashara na Wahasibu Kutoka Halmashauri za Wilaya ya Iramba, Mkalama, Singida Dc, Tandaimba, Bariadi,Kalambo, Kishapu, Madaba, Manyoni, Mbozi,Ikungi, Itilima na Itigi. Mafunzo hayo yameongeza chachu ya ufanisi wa kazi Halmashauri husika kwani zimesaidia kuondoa changamoto mbalimbali zinahusu mfumo wa ukusanyaji wa mapato.
Mafunzo haya ni mwendelezo wa kujengewa uwezo juu ya matumizi bora ya mfumo wa kukusanyia mapato katika serikali za mitaa.mafunzo hayo yameanza mapema tangu mwezi septemba chini ya wawezeshaji kutoka ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI)
Mafunzo haya yamekuwa yakitolewa kwa awamu ambapo inatarajiwa mpaka wataalam hao kumaliza mafunzo watakuwa na uwezo wa kutatua changamoto za mfumo huo na kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani kwa asilimia 100.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa