Mafunzo ya Matumizi ya POS kwa wakusanya mapato ya Halmashauri ya Ikungi
Posted on: January 1st, 2019
Mkurugenzi Mtendaji Ndg, Justice L. Kijazi akizungumza jambo na wakusanya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi juu ya Umuhimu wa kukusanya Mapato. Mafunzo hayo yalitolewa 27-28/12/2018 kwa Awamu ya kwanza. Aidha alisisitiza kuwa Halmashauri inategemea makusanyo ya ndani hivyo Watendaji hao wanapaswa kuwa waadilifu katika suala zima la kukusanya mapato. Alikemea vikali kwa baadhi ya watendaji wanaokusanya fedha za serikali na kuzitumia. "Ni kosa kubwa kutumia fedha za Serikali kabla ya kupelekwa Benki. Pesa ya serikali inapaswa kupelekwa Benki na Matumizi ya pesa yanatakiwa kufuata taratibu na sheria za matumizi ya pesa za Serkali." Alisema.
Alisema kuwa kwa Watendaji waliotumia Pesa za Serikali wanatakiwa kuzirudisha mara moja ndani ya siku 14 na baada ya hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao waliotumia pesa hizo
Naye Afisa Utumishi Ndg, Joseph Hayumu alisisitiza juu ya watumishi wa Umma kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kazi
Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza kushoto akiwa na baadhi ya watendaji wa ofisi, wakisikiliza masomo kwa makini yaliyokuwa yakifundishwa na Maafisa Tehama Bi Eva Myula na Amour Eljabry
Washiriki wa mafunzo ya matumizi ya POS wakisikiliza masomo kwa makini