Afisa Nyuki Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi bwana Philbert Benedict akishirikiana na wataalamu wengine watoa mafunzo juu ya mbinu za ufugaji Nyuki kibiashara katika kutekeleza mradi wenye jina "Kuwezesha ufugaji Nyuki katika vijiji kumi vinavyozunguka msitu wa Minyughe kwa uboreshaji wa kipato ili kupunguza uharibifu wa hifadhi ya msitu wa Minyughe uliopo Wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.Mafunzo hayo yametolewa Kuanzia Tarehe 30 mpaka 31 Januari mwaka huu katika kijiji cha Mnyange na Iglansoni ambapo mafunzo hayo yanalenga kukuza mbinu za ufugaji Nyuki kibiashara na yametolewa kwa vikundi viwili vyenye jumla ya washiriki 60."Vikundi hivyo viwili ni kutoka Kata ya Iglansoni kwa maana ya Vijiji viwili ambavyo ni Iglansoni na Mnyange washiriki 30 kutoka katika kila kikundi na mafunzo yalifanyika kwa nyakati tofauti"amezungumza Afisa NyukiAfisa Nyuki ameongeza na kusema kuwa mradi huo unafadhiliwa na Mfuko wa misitu Tanzania (TaFF) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.Sambamba na hilo Afisa Nyuki ametaja Vijiji hivyo kumi ambavyo vitafikiwa na mradi huo kuwa ni pamoja na Iglansoni, Mnyange, Ng'ongosoro, Muhintiri, Makilawa, Mtavira, Mtunduru, Germani, Mwaru na Mpugizi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa