Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imetenga takrini milioni 600 kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 za wanawake, vijana na walemavu ili kuwainua wananchi kiuchumi kupitia vikundi mbalimbali vifakavyokopeshwa.Hayo yamesemwa wakati wa kufunga mafunzo ya utengenezaji bidhaa mbalimbali za wajasiriamali ikiwa ni pamoja na mafuta ya kupaka, sabuni na vipodozi yaliyofanyika kiwilaya kijiji cha Ikungi chini ya wawezeshaji kutoka chuo cha Arizona kilichopo Dar es Salaam wakishirikiana na halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Afisa maendeleo ya Jamii Bi Haika Massawe amesema kuwa mafunzo hayo ni chachu kwao kuongeza ufanishi kuweza kujiajiri na hata kutengeneza vikundi ili Halmashauri kuwawezesha pindi dirisha la fedha hizo litakapofunguliwa lengo ni kuwainua wananchi kiuchumi na kuondona na adha mbalimbali.
Kwa upande wake muwezeshaji Ndg. Richard Kabaka amewapongeza wanafunzi katika mafunzo hayo kwani ameshirikiana nao kwa karibu kuhakikisha wanaifikia adhma yao.Ameongeza na kusema kuwa anaushukuru uongozi wa halmashauri ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi mtendaji kwani amewapa fursa ya wao kuja na kutoa elimu katika halmashauri yake na kuahidi kushirikiana nao kwa karibu ili elimu hiyo iwafikie watu wengi zaidi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa