Mnamo Tarehe 26 Septemba 2023 Mwenge wa Uhuru ulitia Nanga Kijiji cha Unyakhanya Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida Ukipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi.Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ikungi ulikimbizwa umbali wa Kilometa 137.7 katika miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2 iliyopo katika sekta za Elimu, Maji, Afya, Mazingira, Barabara, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii na ilizindulia,kutembea,na kuweka mawe ya msingi katika miradi hiyo.Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Maji Kijiji cha Matare, Mradi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu 6 ya vyoo Shule ya Msingi Matare,Mradi wa Ujenzi wa barabara,Mradi wa Ujenzi wa kituo kipya cha Mabasi,mradi wa kitalu cha miti, Mradi wa ujenzi wa Wodi ya Wanaume, Wanawake, Watoto na Jengo la kuhifadhia maiti, mradi wa ufyatuaji tofali wa kikundi cha Vijana Chapakazi, program ya kupambana na Rushwa, Malaria, Dawa za kulevya na Kushiriki Usafi wa Mazingira na upandaji miti Kijiji cha Puma.Pamoja na kupita katika Miradi ya Maendeleo,Mwenge wa Uhuru wa Mwaka huu umebeba Ujumbe unaolenga kuwaelimisha na kuwahamasisha Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika harakati za kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo vya maji kama hatua muhimu ya kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabia za nchii, chini ya kauli mbiu isemayo; “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa’’.Aidha,Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii ya Watanzania kuhusu umuhimu na uzingatiaji wa Lishe Bora, Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za Kulevya na Mapambano dhidi ya malaria.Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wamesema kuwa wataendelea kushirikiana vyema na Serikali Inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wanatatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuwaletea Maendeleo Ikungi.MWISHOAfisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi 09/10/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa