Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Kastori Msigala afanya ziara katika kata ya Ighombwe na Mtunduru kukagua miradi ya maendeleo na kufuatilia ukusanyaji wa mapato katika maeneo hayo.
Hayo yamefanyika tarehe 11 Juni, 2025 alipotembelea ujenzi wa matundu matano ya vyoo katika shule ya Sekondari Ighombwe, ukamilishaji wa boma moja la chumba cha darasa katika shule ya Awali na Msingi Msosa, ukamilishaji wa Zahanati ya kijiji cha Makhonda, ujenzi wa darasa moja shule ya msingi Ighombwe, ukamilishaji wa maboma mawili ya maabara katika sekondari Ighombwe pamoja na ukaguzi wa hali ya ukusanyaji wa mapato kijiji cha Masweya kata ya Mtunduru.
Mkurugenzi Mtendaji amesema kuwa adhma ya Halmashauri ya Ikungi ni kukusanya mapato yakutosha ili kuinua maendeleo katika jamii na kukuza uchumi wa wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa