Mh. Rais John Pombe Magufuli azindua Kiwanda cha mafuta Mount Meru Millers
Posted on: March 11th, 2018
Rais Magufuli leo hii anazindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti mkoani Singida Mount Meru Millers baada ya kutoka mkoani Geita akiwa anazindua miradi mikubwa ya barabara.
Mh. Rais ameandamana na Waziri wa viwanda na biashara Mh Charles Mwijage. Mkoa wa Singida una viwanda 543 lakini kiwanda kikubwa ni kimoja tu.
Rais Magufuli amesema kuwa Waagizaji wa mafuta ghafi kutoka nje wamekuwa wakifanya ushawishi kwa wabunge ili kupunguziwa kodi au kutokulipa kabisa
Kutokana na mchezo huo aliouita kuwa mchafu ameziagiza mamlaka husika kutoka kodi kubwa kwa mafuta ghafi yanayoagizwa
Rais Dkt. Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea eneo ambalo watakula raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa mkoa wa Singida muda mchache kabla ya kukizindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti Mount Meru Millers kilichojengwa mkoani humo.