Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson amezindua programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM-2021/22-2025/26) katika Wilaya ya IkungiAkizungumza kabla ya uzinduzi huo leo tarehe 07 Februari 2024 amesema uzinduzi huu kiwilaya ni mwendelezo wa kuimarisha utekelezaji wa program jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ambayo ilizinduliwa rasmi tarehe 13 Desemba, 2021 ili kutekeleza na kuleta matokeo chanya kwa Taifa letu"Hii ni kielelezo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kujielekeza kwenye kuweka misingi imara zaidi ya malezi na makuzi ya watoto wa Taifa hili ili watoto waendelee kukuwa katika utimilifu wao kuanzia hatua za awali za ukuaji wao pia program hii inalenga kutoa afua stahiki kwa watoto wenye Ulemavu ili kuondoa au kupunguza athari za makali kwa watoto wenye Ulemavu na hivyo kuwa na fursa pana zaidi za kufika mbali katika kutoa mchango wao kwa taifa lao", amesema Mkuu wa Wilaya Ndg Justice Kijazi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amesema kuwa vitendo vya Ukatili havikubaliki na ndio maana Sheria kali imekuwa ikichukua mkondo wake kwa wale wanaobainika kufanya vitendo hivi"Hivyo ni jukumu letu kama viongozi kuchukua hatua panapotokea matendo ya kikatili hasa kwa watoto wadogo",amezungumza MkurugenziKwa upande wake Beatrice Maeda Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ikungi ameongeza na kusema kuwa atashirikiana vyema na viongozi wa kata Vijiji na vitongoji kuhakikisha Elimu inafika kuepusha na kubaini vitendo viovu vinavyopeleka ukatili hasa Kwa watoto.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa