Mkuu wa Wilaya ya Ikungi awataka viongozi wa kata,vijiji na vitongoji kusikikiza na kutatua kero za wananchi pindi zinapowakabili ili kuepusha mikwaruzano baina yao.Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo leo Tarehe 23 Octoba 2023 wakati wa ukamilishaji wa utatuzi wa mgogoro wa mpaka baada ya uanishaji wa mpaka kati ya kata ya lighwa na kata ya Dung'unyi Wilayani Ikungi.Mhe Apson amesema ipo haja ya pande mbili kujua mipaka yao iliyoainishwa kisheria ili kuondoa mgogoro huo ambao unasababishwa na kutokua na uelewa mzuri juu ya uwepo wa mipaka ya ardhi kati ya kijiji na kijiji au kata na kata nyingine.Mara baada ya hilo Mhe Apson amepata wasaa wa kutembelea Mradi wa uboreshaji shule kongwe Ujaire shule ya msingi ambapo zaidi ya Milioni 40 zinatumika kujenga madarasa mawili na Ofisi ya Walimu lengo ikiwa ni kuboresha shule kongwe ziweze kudumu zaidi.Mhe Apson ameomba kuongezwa kwa mafundi katika ujenzi wa mradi huo ambao kwasasa upo hatua ya upauaji ili kumalizika kwa wakati "Nataka angalau kila darasa liwe na mafundi watano,wengine wanafunika bati wengine wanamalizia ndani hii ndio kasi Mama yetu Dkt Samia Suluhu anataka ili fedha zingine za maendeleo zije."amesema Mkuu wa Wilaya Ikungi.Imetolewa na:Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi23/10/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa