Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi ameviomba vikundi vya wanufaika wa mkopo unaotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani asilimia 10 (10%) katika wilaya ya Ikungi kutumia vizuri mikopo hiyo ili iweze kuwanufaisha na kuondokana na umasikini...
Akizungumza mara baada ya kusaini mikataba ya makubaliano baina ya halmashauri ya wilaya Ikungi pamoja na wanufaika wa mikopo huo Ndg Kijazi amesema kuwa serikali imetambua na imeona vyema kutenga asilimia kumi ya mapato kuwakoposhe vikundi vya wanawake,vijana pamoja na watu wenye uhitaji maalumu (walemavu) ili kuwakwamua kiuchumi."Hivyo mnapopata mkopo kumbukeni kurudisha kwa wakati mliopewa ili kuwezesha wengine kukopa na kutengeneza uaminifu zaidi" alisema Mkurugenzi Kijazi...
Kwa upande wake Afisa maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe amewapongeza waliojitokeza kuomba mkopo kwani adhima ya serikali ni kukuza kipato cha mwananchi kwa njia ya kutoa mikopo hii kadri mapato ya halmashauri yatakavyopatikana...
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Aliy J.Mwanga ameongeza na kusema serikali haitosita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokiuka makubaliano ya mkataba wa mkopo huo kwani inajitahidi kutenga asilimia 10 kuhakikisha wananchi wananufanika hivyo kwenda kinyume ni kurudisha nyuma wale wenye nia njema na mkopo huu.
MWISHO
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
07/02/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa